NBC Premier League, JKT Tanzania vs Simba SC kupigwa usiku

NBC Premier League burudani inaendelea na Jumamosi, Novemba 8,2025 kutakuwa na mechi mbili kazi kwa wababe kusaka pointi tatu muhimu.

Novemba 8, saa 10:00 jioni Pamba Jiji FC watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba wakiwakaribisha Singida Black Stars ambao tayari wameshawasili Mwanza kwa kazi.

Saa 1:00 usiku, JKT Tanzania watakuwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kumenyana na Simba SC.

Jumapili Novemba 09, 2025 mabingwa watetezi Yanga SC watakuwa Uwanja wa KMC Complex watamenyana na KMC FC.

Saa 1:00 usiku, Namungo FC Uwanja wa Majaliwa dhidi ya AzamFC.

Burudani hii itakuwa mbashara kupitia AzamSports1HD.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.