JKT Tanzania vs Simba SC, pointi tatu kwenye msako

JKT Tanzania vs Simba SC ni mchezo wa ligi unaofuata ikiwa ni msimu mpya wa 2025/26 kwa wababe wawili kusaka pointi tatu muhimu.

Novemba 8,2025 kazi kubwa itafanyika kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu Uwanja wa Mej Jenerali Isahmuyo.

Katika mchezo uliopita msimu wa 2024/25, Simba SC ikiwa ugenini ilivuna pointi kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Fabrince Ngoma ambaye hayupo kwenye kikosi cha mnyama msimu huu.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuwa imara hesabu zao ni kupata pointi tatu.

“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari na maandalizi ambayo tumefanya kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,”.

JKT Tanzania kwenye msimamo wa ligi ni nafasi ya 5 ikiwa na pointi 7 baada ya mechi 5, ushindi mchezo mmoja na sare katika mechi 4.

Simba SC ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 6 baada ya mechi mbili ilipata ushindi katika mechi zote ilizoshuka uwanjani ikiwa nyumbani, huu utakuwa mchezo wa kwanza ugenini.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.