CLEMENT Mzize mshambuliaji wa Yanga SC ataukosa mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex.
Nyota huyo anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki kati ya 8 mpaka 10 baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti ambalo lilikuwa linamsumbua.
Kutokana na hali ambayo anaendelea nayo kwa sasa ni wazi kwamba atakosekana katika mchezo wa ligi kati ya Yanga SC vs KMC FC unaotarajiwa kuchezwa Novemba 9,2025 saa 10:00 jioni.
Mzize alikosekana pia katika mchezo uliopita wa Yanga SC vs Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Oktoba 28,2025.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kwa sasa katika eneo la ushambuliaji wanamtumia Prince Dube ambaye bado hajarejea katika ubora wake.
Dube alianza kikosi cha kwanza mchezo uliopita na alikwama kukamilisha dakika 90. Katika mchezo huo Yanga SC ilishinda kwa mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Zimbwe Jr na Ecua.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.