Simba SC vs TRA United kitaumana Oktoba 30,2025

Simba SC itakaribishwa na TRA United kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Oktoba 30.

Ofisa Habari wa TRA United, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kuwakabili wapinzani wao kuelekea mchezo huo na maandalizi yapo tayari.

Viingilio kwenye mchezo wa Oktoba 30 ni 20,000 VIP na mzunguko ni 10,000 ambapo tiketi ziapatikana ofisi ya TRA Tabora, Big Brother, Uhaziri na TTCL.

Mwangala amewaomba mashabiki kununua tiketi mapema na kutoa sapoti kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Mashabiki ni muhimu kujitokeza kwa wakati na kununua tiketi kwenye vituo ambavyo vimetajwa ili kuisapoti timu,”.

Mchezo uliopita TRA United iligawana pointi mojamoja dhidi ya Mashujaa FC ilikuwa Oktoba 22,2025, ubao wa Ali Hassan Mwinyi uliposomaTRA United 0-0 Mashujaa FC.

Kwa upande wa Simba SC tayari wamewasili Tabora kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.