Mwezi Oktoba kila mwaka, dunia nzima huungana kwa ajili ya matumaini, mapambano, na upendo. Kwa kampuni ya Meridianbet, huu si mwezi wa alama tu, bali ni muda wa kutekeleza matendo halisi yanayogusa maisha ya watu, hasa wanawake wanaopambana dhidi ya saratani ya matiti.
Kupitia mpango wao wa kijamii unaoitwa “Tuko Pamoja Nanyi”, Meridianbet imeendelea kuwa nguzo ya msaada kwa jamii, ikiendesha kampeni za bure za uchunguzi wa saratani ya matiti katika mataifa mbalimbali. Huu ni mradi unaolenga kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma, kuhakikisha kila mwanamke anaweza kufanyiwa uchunguzi bila malipo.
Mfano halisi ni simulizi ya mwanamke mmoja kutoka Montenegro, ambaye alipokea huduma hiyo bila taratibu ngumu bali kwa heshima na urahisi. Hadithi yake ni kielelezo cha namna Meridianbet inavyoweka utu na huruma katikati ya kila mpango wake.

Meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kampeni hii ni sehemu ya jitihada pana za Meridianbet chini ya mwavuli wa Golden Matrix (NASDAQ: GMGI), inayotekeleza miradi ya uwajibikaji wa kijamii katika nchi 18 duniani. Kupitia mfumo wa kidijitali wa Meridian Donate, wachezaji sasa wanaweza kuchangia miradi ya kijamii kwa urahisi, iwe ni hospitali, elimu, au mazingira, kwa kutumia QR code au kupitia mfumo uliopo kwenye michezo wanayofurahia kila siku.
Kwa mfumo huu wa ubunifu, michezo ya kubahatisha imegeuzwa kuwa jukwaa la mabadiliko. Kila mchezo unakuwa fursa ya kutoa, na kila dau linakuwa daraja la matumaini.
Takwimu zinaonyesha ukuaji wa kasi wa athari za kijamii. Mwaka 2024 pekee, Meridianbet ilitekeleza zaidi ya miradi ya kijamii 293, ikisaidia mashirika 212 kupitia kampeni 43 likiwa ni ongezeko kubwa kutoka mwaka uliopita. Wafanyakazi wa kampuni nao wamekuwa sehemu ya safari hii, wakijitolea zaidi ya saa 5,000 kushiriki moja kwa moja katika miradi ya kusaidia jamii.
Tangu kuanzishwa kwa Meridian Foundation mwaka 2020, zaidi ya vituo 40 vya afya vimenufaika kupitia misaada ya moja kwa moja, huku miradi mipya kama kampeni ya kuchangia vitabu ikileta faraja kwa shule na maktaba zenye uhitaji mkubwa. Ndani ya muda mfupi, maelfu ya vitabu vimekusanywa na kusambazwa katika nchi zote 18 ambako Meridianbet inafanya kazi.
Kwa Meridianbet, uwajibikaji wa kijamii haupimwi kwa maneno, bali kwa matokeo. Ni imani yao kwamba teknolojia inaweza kuwa chombo cha upendo, na michezo inaweza kuwa njia ya kusaidia wengine.