Yanga SC imepata ushindi wa mabao 2-0 Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Oktoba 28,2025 wababe hao wawili walikutana kusaka pointi tatu, Mtibwa Sugar waliingia kwa mbinu ya kujilinda zaidi hali iliyofanya wachezaji wa Yaga SC kufanya majaribio mengi wakiwa nje ya 18 ambayo yalifanikiwa kuzama kambani.
Mabingwa watetezi Yanga SC wamebeba pointi tatu na beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr ametwaa tuzo ya mchezaji bora katika mchezo wa leo wa ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Zimbwe Jr alifunga bao hilo akiwa nje ya 18 kwa shuti kali kwa mguu wake wa kushoto akitumia pasi ya Duke Abuya.
Bao la pili lilifungwa na Celstin Ecua dakika ya 83 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.
Zimbwe Jr amesema kuwa ni furaha kuona timu inashinda na yeye kuchaguliwa kuwa mchezaji bora ni sehemu ya ushindi wa timu kiujumla.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.