Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League, ni matokeo ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25,2025.
Ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Yanga SC kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya makundi kwa msimu wa 2025/26 baada ya ule wa ugenini Oktoba 18,2025 kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Mabao yote ya Yanga SC yalifungwa kipindi cha kwanza yalitosha kuwapa tiketi wawakilishi wa Tanzania kusonga mbele mpaka hatua ya makundi Afrika.
Ni Dickson Job alifungua pazia la kufunga dakika ya 6 kwa asisti ya Doumbia ambaye alipiga kona baada ya Duke Abuya kufanya jaribio akiwa nje kidogo ya 18.
Pacome Zouzoua ambaye alikuwa kwenye kiwango bora alifunga bao la pili dakika ya 34 asisti ya Maxi Nzengeli.
Yanga SC inatinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 na ilipewa zawadi ya goli la mama milioni 10 mara baada ya mchezo huo kukamilika na mashabiki walijitokeza wengi kuishangilia timu hiyo.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.