Yanga SC vs Silver Strikers hesabu zimeanza mapema

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa unaamini utafanikiwa kuandika historia kwa kutinga hatua ya makundi kwa kupata ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya Silver Strikers.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 18, 2025 matokeo yalikuwa Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League mchezo uliochezwa Uwanja wa Bingu.

 Goli la ushindi lilifungwa dakika ya 76 na Andulu Yosefe na mchezo mmoja wa maamuzi utachezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25,2025 huu utaamua nani atatinga hatua ya makundi.

Walter Harson, Meneja wa Yanga SC ameweka wazi wanaamini wataandika historia Jumamosi kwa kutinga hatua ya makundi licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Silvers Strikers.

“Hii ni Champions League tunakwenda kuandika historia kwenye mchezo wa Jumamosi ambapo tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kutinga hatua ya makundi.

“Mashabiki watambue kwamba matokeo ya mchezo uliopita hayo yamekwisha hivyo kwa sasa tunafanya maandalizi kwa mchezo wetu ujao,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.