Simba SC vs Nsingizini Hotspurs ukurasa ndo kwanza uaanza licha ya mchezo wa ugenini uliochezwa Oktoba 19,2025 mnyama kupata ushindi wa mabao 3-0 mchezo ulichezwa Uwanja wa Somholo,
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema bado hawajatinga hatua ya makundi kutokana na ugumu wa kila mchezo CAF Champions League hivyo ni jukumu la mashabiki kuendelea kujipanga kuelekea mchezo ujao.
Ahmed amesema: “Tumepata ushindi wa mabao 3-0 ugenini haikuwa kazi rahisi tunawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa ambayo wameifanya na namna ambavyo wamekuwa imara katika kutimiza majukumu yao.
“Haya matokeo ni zawadi kwa mashabiki wa Eswatini, hawa Nsingizni sio timu ya kubeza hata kidogo kazi haijaisha, kuelekea kwenye mchezo wetu wa Jumamosi tuna kazi ya kupambana kupata ushindi upya kwa ajili ya mashabiki wa Dar,”.
Mabao ya Simba SC kwenye mchezo huo yalifungwa dakika ya 45 ya mchezo, kupitia kwa beki Wilson Nangu akitumia kona ya Neo Maema. Kibu Dennis dakika ya 82 alifunga goli la pili kwa pasi ya Jonathan Sowah na alifunga goli la tatu dakika ya 89 kwa pasi ya Morice Abraham.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.