FOUNTAIN Gate inayotumia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kwa mechi za nyumbani inakuja na tamasha kubwa ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 12 2025 ikiwa ni utambulisho kwa benchi la ufundi na wachezaji.
Ikumbukwe kwamba tayari Fountain Gate imezindua uzi mpya kwa msimu wa 2025/26 Oktoba 10 2025 katika mechi za mwanzo za ligi ilianza kwa kupoteza dhidi ya Mbeya City wakiwa nyumbani.
Ofisa Habari wa Fountain Gate, Issa Mbuzi amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na wanakuja lenye kauli mbiu ya Tumejipata, Tunaanza na Mungu.
“Tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya licha ya mwanzo kuwa mbaya kwetu tunaamini tunarejea kwenye ubora kutokana na maandalizi ambayo tunayafanya.
“Tuna jambo letu ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 12 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Babati, mashabiki wajitokeze kwa wingi tunakuja na kauli mbiu ya Tumejipata, Tunaanza na Mungu,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.