TIMU ya taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco imepoteza kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Zambia katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan Oktoba 8 2025.
Goli pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 75 mfunganji Fashion Sakala akitumia pasi ya Lubambo Musonda likiwapa Zambia nafasi ya kuongoza.
Goli hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuifanya Tanzania kupoteza matumaini kufuzu Kombe la Dunia.
Kwenye mchezo huo jumla ya kadi tano za njano zilitolewa huku kwa Tanzania ni wachezaji watatu wakionyeshwa na kadi wawili zikionyeshwa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia.
Bakari Mwamnyeto dakika ya 56, Yahya Omary dakika ya 30 na kiungo Feisal Salum dakika ya 33 walionyeshwa kadi za njano kwa upande wa Tanzania. Lawarence Mulega dakika ya 89 na Benson Sakala dakika ya 78 walionyeshwa kadi kwa upande wa timu ya Zambia.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.