Simba SC imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba Mosi 2025.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Chamou Karabou dakika ya 43 akitumia pasi ya Joshua Mutale ambaye aligipa kona, dakika ya 60 kupitia kwa Rushine De Reuck ambaye alimalizia kazi ya faulo iliyopigwa na Maema, Seleman Mwalimu alifunga bao la tatu dakika ya 84.
Nyota wa mchezo amechaguliwa beki Rushine ambaye kwenye mechi mbili mfululizo za ligi amefunga ilikuwa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Fountain Gate na mchezo wa pili dhidi ya Namungo FC yote ikichezwa Uwanja wa Mkapa.
Simba SC inafikisha jumla ya pointi 6 kibindoni inaongoza ligi kwa idadi ya mabao 6 ambayo imefungwa inalingana pointi na Singida Black Stars ambayo ilitoka kupata ushindi wa ba0 1-0 dhidi ya Mashujaa FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC. Bao la Singida Black Stars lilifungwa na Elvis Rupia ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.