Nasreddine Nabi kuifundisha Simba SC?

JINA la Nasreddine Nabi aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC na kuipa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara linatajwa kuwa katika orodha ya wale wanaoipigiwa hesabu kupewa mikoba ya Fadlu Davids ndani ya Simba SC.

Kwa sasa Simba SC ipo kwenye mchakato wa kumtafuta kocha mpya baada ya Fadlu Davids kupata changamoto nyingine katika timu ya Raja Casablanca.

Inaelezwa kuwa Nabi yupo kwenye ardhi ya Tanzania akiwa hapa kwa muda zaidi ya siku tatu huku ikielezwa kwamba safari yake ni kuja kukamilisha mazungumzo na Simba SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa hajui jambo lolote kuhusu Nabi kuwa Tanzania kwa kuwa suala la kumtafuta kocha uongozi wa juu unalifanyia kazi.

“Ndugu zangu waandishi wa habari kuhusu Nabi kuja kuifundisha Simba SC sijui jambo lolote ila nachujua ni kwamba huyo ni kocha mzuri kutokana na uzoefu alionao na alifanya kazi nzuri kwenye ligi.

“Alichukua makombe nadhani kama mawili hivi hivyo sio kocha wakumbeza uwezo wake ni mzuri, kama yupo Dar hilo mimi sijui na ningekuwa najua kwamba anakuja kuifundisha Simba SC nisingewaficha kitu ningewaambia ndugu zangu.”

Simba SC Oktoba Mosi 2025 ilicheza mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC ilipata ushindi wa mabao 3-0 kwenye benchi alikuwa ni Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.