Hizi hapa mechi tatu za Romain Folz Yanga SC

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 Yanga SC wana dakika 270 za kazi ndani ya Oktoba kwa mechi tatu za ushindani uwanjani.

Hizo ni mechi tatu za kazi kwa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi sita bila kuambulia kipigo.

Kwenye mechi hizo sita, tanoFolz alishuhudia Yanga SC ikishinda na mechi moja walitoshana nguvu ilikuwa dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 30 2025.

Katika mechi hizo tatu, watacheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi mchezo wa kwanza itakuwa ugenini Malawi kati ya tarehe 17-19 na ule wa marudiano utapigwa nyumbani kati ya tarehe 24-26.

Mchezo mmoja ni wa ligi ya NBC itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar Oktoba 29 2025 Uwanja wa Mkapa katika msako wa pointi tatu muhimu.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.