Usiku wa leo, anga la soka barani Ulaya linawaka moto wa ushindani, huku UEFA Champions League ikirudi tena na msimu mwingine wa mechi tisa za kuvutia. Mashabiki wa Meridianbet na wapenda kubashiri wanatarajia burudani ya hali ya juu, huku kila mchezo ukiwa na hadithi yake, ladha yake, na nafasi ya kuandika historia mpya.
Vita ya uwanja wa nyumbani inawaka aswa, ambapo Qarabag wanawakaribisha Copenhagen. Wenyeji wanatafuta kuonyesha ubabe wao, lakini wageni kutoka Denmark hawajaja kutalii, wana uzoefu wa kutosha kwenye jukwaa la Ulaya. Odds za Meridianbet zinatoa nafasi ya ushindi wa kipekee kwa wabashiri.
Baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Barcelona, Newcastle wanatua Ubelgiji kwa lengo moja tu, kuondoka na pointi tatu. Lakini Gilloise si wa kubezwa, walishangaza wengi kwa ushindi wao wa awali. Mechi hii ni fursa, na Meridianbet iko tayari kukuongezea nguvu ya ushindi.
Bila kusahau, Meridianbet ina michezo ya kasino mtandaoni na mechi mbalimbali kubwa zenye odds za kuvutia kila siku. Jiunge sasa kupitia meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
AS Monaco dhidi ya Manchester City ni mechi ya hadhi ya kifalme. Monaco wanakumbuka kwa furaha msimu wa 2016/17 walipowatoa City kwa kipigo cha 3-1. Lakini vijana wa Guardiola leo wanakuja na kikosi kilichoshiba ubora wa viwango vya Dunia. Ni mtanange wa kulipiza kisasi au kuendeleza rekodi?
Vilevile, The Gunners wanahitaji ushindi wa nyumbani dhidi ya Olympiacos ili kuondoa kumbukumbu ya kipigo kutoka kwa Wagiriki hawa. Olympiacos wamewahi kuwanyamazisha Emirates, na leo wanarudi kwa lengo lilelile. Odds ni tamu kwa mbashiri mwenye ujasiri.
Barcelona na PSG uwanjani pale Nou Camp. Hii ndiyo mechi ya siku sasa. Mashabiki bado wanakumbuka La Remontada ya 2017, lakini PSG wa sasa si wale wa jana, kikosi kipya, kasi mpya, wakiwa ni mabingwa watetezi na mastaa wenye njaa ya ushindi.
Dortmund wanarudi nyumbani kuwakaribisha Athletic Club baada ya comeback ya kuvutia dhidi ya Juventus. Lakini Athletic Club si wageni wa presha, wana nidhamu na mbinu za kuzuia. Mechi hii ni ya kiufundi, na Meridianbet ina odds zinazovutia kwa mbashiri makini.
Napoli wanapiga hatua kwa rekodi nzuri ya nyumbani, lakini wanacheza na Sporting CP ambao wana mbinu za kisasa na nidhamu ya hali ya juu wakiwa ugenini. Mabao yanatarajiwa, na burudani ni uhakika.
Juventus wanahitaji ushindi dhidi ya Villarreal baada ya suluhu kwenye mchezo wa kwanza wa Uefa ili kurejesha imani kwa mashabiki, lakini Villarreal wamekuwa wagumu nyumbani na wana uhitaji wa alama hizi kwani wao pia walipoteza mchezo wa awali. Ni mechi ya kubashiri kwa ushindi mkubwa.
Usiku huu ni usiku wa burudani tupu, hisia kali, na fursa ya kipekee kwa mashabiki na wabashiri kufurahia kila sekunde. Ukiwa na Meridianbet, kila mechi ni nafasi ya ushindi.