Mbeya City vs Yanga SC, kiungo wa kazi arejea kazini

KIUNGO Mohamed Doumbia wa Yanga SC anatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City baada ya kuwa nje kutokana na kutokuwa fiti.

Katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete ya Angola nyota huyo alikosekana Uwanja wa Mkapa.

Sababu kubwa ilikuwa ni maamuzi ya benchi la ufundi kuamua kumpumzisha ilia pate matibabu zaidi. Tayari ameshakuwa katika uimara.

Katika mazoezi ya mwisho ya Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz, Septemba 29 2025 Mbeya alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika uwanja wa mazoezi.

Yanga SC inatarajiwa kumenyana na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Septemba 30 2025.

Utakuwa ni mchezo wa pili kwa Yanga SC ambayo ilifungua pazia kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mbeya City mchezo wake uliopita wa ligi ilitoka kupoteza ugenini kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.