Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Sokoine
Septemba 30 2025
FT: Mbeya City 0-0 Yanga SC
Mbeya City inagawana pointi moja na mabingwa watetezi Yanga SC katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho. Eneo la kuchezea limekuwa ni changamoto kwa wachezaji wote wa timu zote mbili wenyeji Mbeya City na wageni Yanga SC.
Zinaongezwa dakika 6
Dakika 90 zimekamilika Uwanja wa Sokoine
Dakika ya 89 Edmund anapiga kona inaokolewa
Dakika ya 89 Edmund John anapiga faulo inakwenda kugonga nguzo na kurudi uwanjani
Dakika ya 88 Stewart anaingia
Dakika ya 88 Ambokile jaribio lake linagonga mwamba
Dakika ya 87 Diarra anaokoa hatari
Dakika ya 87 Kakolanya anaokoa hatari kwa Mbeya City
Dakika ya 86 Mbeya City wanakutwa kwenye mtego wa kuotea
Dakika ya 83 Boyel anacheza faulo kwa nyota wa Mbeya City
Dakika 81 Doumbia anarusha
Dakika ya 80 Dube anaingia
Dakika ya 75 Vitalis Mayanga anacheza faulo
Dakika ya 73 Edmund John anapiga kona ambayo haiwi faida kwa Yanga SC
Dakika ya 69 Ame anaokoa hatari
Dakika ya 68 Maxi anatoka anaingia Edmund John
Dakika ya 68 Kouma anaingia anachukua nafasi ya Duke
Dakika ya 68 Peter anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 63 Pacome anapiga faulo
Dakika ya 62 Duke anachezewa faulo
Dakika ya 61 Job anachezewa faulo
Dakika ya 60 Doumbia anakwenda nje anaingia Ecua
Dakika ya 60 Maxi amacheza faulo
Dakika ya 58 Pacome anapoteza pasi ndani ya 18
Dakika ya 58 Peter Samson anatoka
Dakika ya 53 Maxi anapiga kona inaokolewa na Beno
Mbeya City 0-0 Yanga SC
Zinaongezwa dakika 3
Dakika ya 45 Andambilwe anapoteza pasi
Dakika ya 44 Kakolanya anaanzisha mashambulizi
Dakika ya 44 Boka anapoteza mpira
Dakika ya 44 Boyel anapoteza mpira
Dakika ya 43 Maxi anapiga kona inaokolewa na Mbeya City
Dakika ya 42 Yahya anaokoa hatari ndani ya 18 iliyopigwa na Pacome
Dakika ya 42 Matheo Anthony anapiga pasi fupi
Dakika ya 41 Vitalis Mayanga anaokoa hatari
Dakika ya 41 Yahya Mbegu anarusha mpira kuelekea Yanga SC.
Dakika ya 40 Bacca anapiga faulo
Dakika ya 39 Andambilwe anapoteza mpira ndani ya 18
Dakika ya 38 Diara okoa hatari
Dakika ya 38 Boyel anakutwa katika mtego wa kuotea
Dakika ya 37 Boka anachezewa faulo
Dakika ya 36 Matheo anamchezea faulo Job
Dakika ya 35 Ame anaokoa
Dakika ya 35 Yahya Mbegu anaokoa hatari
Dakika ya 34 Diara anaanzisha mashambulizi kuelekea Mbeya City
Dakika ya 34 Andambilwe anapokwa mpira
Dakika ya 33 Mbeya City wanapiga faulo
Dakika ya 32 Bacca anamchezea faulo Matheo Anthony
Dakika ya 32 Doumbia anafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 31 Maxi anarusha
Dakika ya 30 Doumbia anacheza faulo
Dakika ya 29 Boka anarusha
Dakika ya 29 Baraka Filemon anaokoa hatari mbele ya Pacome
Dakika ya 28 Pacome anapiga kona, mwamuzi Omary Mdoe anaruhusu ipigwe kona
Dakika ya 27 Doumbia anapiga pasi fupi kwa Pacome
Dakika ya 27 Pacome anapiga kona, Mbeya City wanaokoa
Dakika ya 27 Pacome anafanya jaribio Baraka anaokoa
Dakika ya 26 Ambokile jaribio lake linaokolewa na Djigui Diarra
Dakika ya 25 Eliud Ambokile anacheza faulo
Dakika ya 24 Pacome anapeleka mashambulizi Mbeya City
Dakika ya 24 Bacca anapiga pasi ndefu
Dakika ya 23 Ibrahim Ame anapiga faulo
Dakika ya 23 Duke anacheza faulo
Dakika ya 22 Maxi Nzengeli anapelekea mashambulizi Mbeya City
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.