Michezo kuwa sehemu ya ajira kwa vijana ni moja ya agenda kubwa inayopigiwa hesabu kukamilika kwa ukubwa katika kata ya Usuka iliyopo wilaya ya Njombe.
Kijana mchapakazi Aliko Delile mgombea wa udiwani kata ya Usuka kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) amebainisha hayo katika kampeni za uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 2025.
Aliko Delile ambaye amekuwa akiwapambania vijana kwenye sekta ya michezo ni mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Usuka ambayo ina vijana wapenda maendeleo, wapenda michezo na watu wanaopambana bila kukata tamaa.
Mgombea huyo amesema kuwa ikiwa atachaguliwa kuwa diwani wa kata ya Usuka atasimamia kwa vitendo shughuli zote za michezo kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa.
“Kwenye upande wa michezo ni miongoni mwa vipaumbele vikubwa ambavyo nitavisimamia kwa ushirikiano na viongozi wengine ili kuona kwamba tunakuwa kwenye ushindani mkubwa.
“Kuna suala la vifaa bora hili litakuwa namba moja, mazingira mazuri katika maeneo ya kuchezea hapa tunazungumzia kuhusu ubora wa viwanja na usalama kwa mashabiki ni kitu cha msingi kwa kata ya Usuka.
“Mbali na michezo ni kuhakikisha kwamba elimu inazingatiwa na wale ambao wanatakiwa kuwa shule itakuwa ni lazima waende shule inakuwa sio jambo la hiari.
“Kwa upande wa elimu ya sekondari ni kuona kwamba inatoka day mpaka boarding na hii inawezekana ikiwa tutashikamana. Pia mpango mkakati ni kubadilisha sekondari yetu kutoka day kuwa boarding inawezekana tukishikamana,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.