YANGA SC imefungua pazi la Ligi Kuu Bara ya NBC kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 24 2025.
Yanga SC ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 45 kufunga bao la uongozi kupitia kwa Kouma ambaye aliunganisha krosi iliyopigwa kwa pigo la kona.
Kipindi cha pili Yanga SC walipata mabao mawili kupitia kwa Maxi Nzengeli ambaye alitumia pasi ya beki Zimbwe Jr.
Hii ni pasi ya kwanza kwa Zimbwe akiwa na uzi wa Yanga SC kwenye mchezo wa ligi msimu wa 2025/26 na alikomba dakika 90 mwanzo mwisho katika mchezo chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz ilikuwa dakika ya 63 alitoa pasi ya bao kwa Maxi.
Kamba ya tatu ni mali ya Mudathir Yahya dakika ya 90 akitumia pasi ya Pacome. Ni Maxi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.