Simba Ushindi wa ugenini si bahati, ni uthibitisho wa ubora

“Ni kweli, mijadala ipo—Simba haikucheza soka la kuvutia sana dhidi ya Gaborone United, lakini bado ikaibuka na ushindi. Wapo wanaoona kama ni dalili za udhaifu, lakini kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kutoa hukumu ya haraka.

Kwanza, Simba walikabiliana na timu bora ambayo ilikuwa imepumzika na kujiandaa kikamilifu kwa mechi hiyo. Pili, Simba wamekusanya pointi tatu muhimu ugenini, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kufanya marekebisho kwenye mchezo wa nyumbani. Tatu, ratiba ya safari zao ilikuwa ngumu mno—kuanzia baada ya mechi ngumu dhidi ya Yanga, kisha safari ndefu hadi Afrika Kusini, Gaborone na baadaye Francistown. Zaidi ya masaa 24 yamepotea angani na viwanja vya ndege, huku muda wa mazoezi na kupumzika ukiwa mdogo sana.

Uchovu ni hali ya kawaida kwa wachezaji katika mazingira kama hayo, na bado Simba waliweza kupambana, kuonyesha nidhamu ya kiufundi na kupata matokeo wanayoyahitaji.

Hii haimaanishi Simba wamemaliza kazi. Safari bado ni ndefu, nafasi ya kurekebisha ipo, na mchezo wa nyumbani ndiyo kipimo cha kweli cha ubora wao.

Jambo la muhimu kwa Wanamsimbazi sasa si kulalamika wala kushusha morali, bali kuwaamini wachezaji wao. Hawa ni wanajeshi waliopambana katika mazingira magumu, na bado wameanza vyema kampeni ya msimu huu wa CAF Champions League.

Safari imeanza, na mshindi huamuliwa mwisho, si mwanzo.” amesema Mchambuzi nguli wa soka nchini, Saleh Jembe kupitia ukurasa wake wa Instagram