KOCHA Mkuu wa Simba SC Fadlu Davids anatajwa kuomba kuondoka ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Fadlu yupo na kikosi nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Gaborone United unaotarajiwa kuchezwa Septemba 20.
Simba SC imetoka kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC. Katika mchezo huo uliochezwa Septemba 16 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC.
Fadlu hajawa na bahati kupata ushindi mbele ya Yanga SC licha ya kuwa na mbinu tofauti kila wanapokutana kwenye mechi za ushindani.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2024/25 kwenye mechi tatu ambazo walikutana akiwa kocha alikwama kupata ushindi. Ilikuwa mchezo wa Ngao ya Jamii na mechi mbili za ligi Simba SC ilipoteza nje ndani.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa akaondoka ndani ya Simba SC baada ya kupata ofa nchini Morocco licha ya kuwa na mkataba ndani ya Simba SC.
Simba SC ina kibarua katika anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo huo watakosa huduma ya beki Hamza aliyepata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.