ZIMEBAKI SIKU MBILI KARIAKOO DABI KWA MKAPA

ZIMEBAKI siku mbili kabla ya mchezo wa Kariakoo Dabi kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 ikiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga SC walitwaa taji hilo kwa ushindi kwenye mchezo wa fainali mbele ya Azam FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Simba SC iligotea kuwa mshindi wa tatu kwa kuwa mashindano hayo yaliendeshwa kwa kuanzia hatua ya nusu fainali.Kwenye hatua ya nusu fainali Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC bao la ushindi likifungwa na Maxi Nzengeli.

Tayari viingilio vimetangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania kuelekea kwenye mchezo huo na Septemba 15 2025 kutakuwa na maandalizi ya mwisho kwa timu zote mbili Yanga SC na Simba SC ambapo mkutano wa benchi la ufundi unatarajiwa kufanyika saa 5:00 asubuhi Uwanja wa Mkapa.

Mzunguko kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ni 5,000 huku safari hii kukiwa na tiketi za Platinum ambazo kiingilio chake ni 300,000, VIP A ni 100,000, VIP B ni 30,000, VIP C 20,000 na Orange ni 15,000.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.