ZIMBWE JR AFIKIRIA MAKUBWA YANGA SC

Mohmaed Hussen Zimbwe Jr beki wa kushoto ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu Romain Folz amesema kuwa anafurahia mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa mashabiki anamini watajituma kufanya vizuri ndani ya uwanja.

Ipo wazi kwamba Zimbwe Jr ni miongoni mwa wachezaji waliopokewa kwa shangwe kubwa ndani ya Yanga SC katika utambulisho wake, beki huyo 2024/25 alikuwa katika kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

“Tamasha limeenda vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mashabiki wamejitokeza wengi na hii ni ishara kuwa huu ni mwanzo mzuri kuelekea katika msimu mpya.

“Kuna vipaji vingi ambavyo vipo ndani ya Yanga SC na nina amini kwamba nami nimeongezeka. Ninashukuru kwa kuwa nipo katika timu ambayo ina talent kubwa.

“Ninaona mbali zaidi kwa kuwa kila mchezaji anaipigania nembo ya timu nami nimeongezeka. Wananchi ninawapenda na nina amini tutakuwa kwenye kazi kubwa kwa ajili ya kufikia mafanikio,”.

Mchezo ujao kwa Yanga SC ni Septemba 16 2025 dhidi ya waajiri wake wa zamani Simba SC. Huu utakuwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii, mchezo maalumu wa ufunguzi wa ligi msimu wa 2025/26 utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.