YANGA SC 1-0 BANDARI

YANGA SC imepata ushindi mbele ya Bandari katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo umekamilika dakika 90 kwa ushindi wa bao 1-0 ambalo limedumu mpaka mwisho wa mchezo kirafiki.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo Ecua dakika ya pili kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya mshambuliaji Prince Dube.

Huu ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Yanga SC Uwanja wa Mkapa na mchezo ujao ni Ngao ya Jamii unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 16.

Mbali na mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa leo kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na washerehesaji tofautitofauti akiwemo Maulid Kitenge.

Kwa upande wa Wasanii Dogo Patern, Zuchu ni miongoni mwa wasanii waliotoa burudani mbele ya mashabiki wengi ambao walijitokeza.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.