MSANII ROSE NDAUKA ANUSURIKA AJALI YA GARI, AMSHUKURU MUNGU!

Msanii wa filamu na muziki, Rose Ndauka, amenusurika katika ajali ya gari na kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rose alishiriki picha za gari lililopata ajali huku akiandika ujumbe mfupi uliojaa shukrani:

“Ahsante sana Mungu kwa kutuonekania siku zote 🙏🙏🙏.”

Ujumbe huo uliwagusa mashabiki wengi ambao walimiminika kwenye ukurasa wake kumpongeza kwa kutoka salama, huku wakimtia moyo aendelee kuwa imara baada ya tukio hilo.

Rose, ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu nchini, amekuwa akipendwa na mashabiki kwa mchango wake katika filamu na muziki wa Bongo, na tukio hili limeacha wengi wakimtakia afya njema na maisha marefu.