Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Septemba 5 2025 kitakuwa kazini kwenye mchezo dhidi ya Congo Brazzaville ambao ni maalumu kwa ajili ya kufuzu kombe la Dunia 2026 utakaochezwa Uwanja wa Alphonce Masamba Debat.
Septemba 4 2025 Stars ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa ambao utatumika kwa mchezo wa leo kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleman.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo katika kikosi cha Stars ni Simon Msuva, Mbwana Sammatta, Dickson Job, Clement Mzize, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Nado, Bacca.
Ikumbukwe kwamba Stars imetoka kushiriki CHAN 2024 ikigotea hatua ya robo fainali na mabingwa walikuwa ni Morocco ambao waliwafungashia virago Stars kwenye hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa.
Septemba 9 2025 Taifa Stars itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Niger ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.