UONGOZI wa Fountain Gate umeweka wazi kuwa upo tayari kwa msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 haukuwa imara kwa timu hiyo ambayo ilianza kwa kasi mzunguko wa kwanza na iliandika rekodi ya kuwa ndani ya tano bora kwa muda mrefu kisha ikaporomoka mpaka kuwa timu iliyocheza Play Off.
Inaingia kwenye orodha ya timu ambazo zilifungwa mabao mengi ndani ya ligi baada ya kucheza mechi 30 ilifungwa jumla ya mabao 58 na ilikusanya pointi 29.
Kwenye msimamo ilimaliza ikiwa nafasi ya 14, ilipata ushindi kwenye mechi 8 sare 5 na ilipoteza jumla ya mechi 17 safu yake ya ushambuliaji ilifunga mabao 32 pekee.
Dirisha la usajili lililofunguliwa Julai Mosi 2025 linatarajiwa kufungwa Septemba 7 2025 huku taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) likiitaja Foutain Gate kuwa katika orodha ya timu ambazo hazijakamilisha usajili hiyo ilikuwa ni Septemba Mosi na timu nyingine ni Coastal Union ya Tanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Fountain Gate, Issa Mbuzi amebainisha kuwa timu hiyo ipo kamili kwa ushindani na imekamilisha usajili wa wachezaji wapya kuelekea msimu wa 2025/26.
“Tupo vizuri na kamili kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26, kuhusu usajili tumefanya usajili mzuri na tumekamilisha masuala ya usajili.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.