KIUNGO WA YANGA SC KUIBUKIA SINGIDA BLACK STARS

NYOTA Clatous Chama inatajwa kuwa amemalizana na Singida Black Stars kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuwa hapo msimu wa 2025/26.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Chama alikuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambapo hapo mkataba wake umegota mwisho kwa kuwa alisaini mwaka mmoja. Alikuwa ni mchezaji wa kwanza kutangazwa kuwa Yaga SC akitokea Simba SC.

Inaelezwa kuwa kiungo huyo amefikia makubaliano mazuri ya kujiunga na timu hiyo, baada ya kumpa dau nono la usajili na mshahara mzuri katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

Awali ilikuwa inatajwa kuwa huenda akajiunga na Zesco United ama Azam FC huko mipango imekuwa tofauti hivyo kuna asilimia kubwa akiwa ndani ya Singida Black Stars.

Nyota huyo ataungana na kiungo mkabaji Khalidi Aucho rai awa Uganda ambaye tayari ametambulishwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars ambacho kitakuwa Dar kwa muda wa mwezi mmoja kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26 na kitashiriki mashindano ya Kagame Cup 2025.

Mchezo wao wa kwanza kwa Singida Black Stars unatarajiwa kuchezwa Septemba 2 2025 itakuwa dhidi ya Ethiopean Coffee, Uwanja wa Azam Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.