SIMBA SC NDANI YA DAR KAMILI KWA SIMBA DAY SEPTEMBA 10

KIKOSI cha Simba SC  kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimewasili salama Jijini Dar es Salaam alfajiri ya saa 11 kikitokea Misri ambako kiliweka kambi ya msimu ujao wa 2025/26.

Baada ya kuwasili kikosi cha Simba SC kinatarajia kuanza maandalizi mapema kuelekea kwenye mchezo wa Simba Day unaotarajiwa kuchezwa Septemba 10 2025 Uwanja wa Mkapa.

Tayari Simba SC imetangaza timu ambayo itacheza nayo mchezo wa kirafiki Septemba 10 2025 ni Gor Mahia ya Kenya hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanasubiriwa kwa shauku ni Ellie Mpanzu ambaye huyu ni winga mwenye nguvu akiwa uwanjani na uwezo wa kumiliki mpira.

Awali ilikuwa inatajwa kuwa huenda akasepa Simba SC lakini bado yupo. Kibu Dennis, Seleman Mwalimu ambaye ni ingizo jipya, Jonathan Sowah ambaye ni mshambuliaji na Jean Ahoua kinara wa kufunga msimu wa 2025/26.

Steven Mukwala mshambuliaji wa Simba SC amesema kuwa ilikuwa ni kambi nzuri kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.

“Ilikuwa ni kambi nzuri na tumefanya kwa uwezo na ushirikiano mkubwa. Tunaamini kwamba utakuwa ni msimu wenye ushindani na tupo tayari mashabiki wawe pamoja nasi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.