MSIMU MPYA WA LIGI KUU BARA KUANZIA SEPTEMBA 17, RATIBA IPO HAPA

Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 17, 2025 kwa michezo miwili ya ufunguzi.

KMC FC wataikaribisha Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge  jijini Dar es Salaam, huku Coastal Union wakifungua pazia lao kwa kuvaana na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TPLB), msimu huu utamalizika Mei 23, 2026, ambapo bingwa mpya wa Ligi Kuu atajulikana.

Msimu wa 2025/26 unatarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi, hasa ukizingatia maandalizi makubwa yaliyofanywa na vilabu vikubwa vya Kariakoo, Simba na Yanga, sambamba na Singida FG na Azam FC ambao wamekuwa na usajili kabambe.

Ratiba kamili ya michezo inatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, lakini tayari shauku kubwa imetanda kwa mashabiki wa soka nchini kuelekea msimu mpya.