FENERBAHÇE YAACHANA NA JOSE MOURINHO BAADA YA MWAKA MMOJA

Klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki imetangaza kuachana na kocha wake, Jose Mourinho, ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kujiunga na timu hiyo. Hatua hiyo inakuja siku mbili baada ya Fenerbahçe kutolewa kwenye hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Ulaya na klabu ya Ureno, Benfica.

Kupitia taarifa rasmi, Fenerbahçe ilisema Mourinho na klabu wameafikiana kuvunja mkataba wao kwa pamoja:

“Tunamshukuru Jose Mourinho kwa juhudi na mchango wake wakati akiwa nasi, na tunamtakia kila la heri katika kazi yake ya baadaye.”