Mshambuliaji Clement Mzize wa Yanga SC ameboreshewa mkataba wake ambapo mshahara wake inatajwa itakuwa ni milioni 40 kwa mwezi akiwa mchezaji mzawa namba mbili kukunja mshahara mrefu.
Namba moja ni Feisal Salum wa Azam FC ambaye inaelezwa kuwa anakunja milioni 50 kwa mwezi.
Agosti 27 2025 Yanga SC wametangaza rasmi kuongeza mkataba na mshambuliaji huyo ambaye msimu wa 2024/25 alifunga mabao 14 kwenye ligi.
Mzize kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2024/25 alicheza mechi 30. Alitwaa ubingwa na kikosi cha Yanga SC ambacho kilikusanya pointi 82. Jina lake lipo kwa wachezaji wat imu ya taifa ya Tanzania iliyoishia robo fainali CHAN 2024.
Rekodi zinaonyesha kuwa alitumia dakika 1,877 kwenye mechi za ligi. Alifunga jumla ya magoli 14 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC. Ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi ndani ya ligi.
Katika CHAN 2024 alifunga magoli mawili. Ilikuwa kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Madagascar. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa na Tanzania ilishinda kwa mabao 2-1.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.