Timu ya Taifa ya Sudan imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024) baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 4–2 dhidi ya Algeria kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa na kumalizika kwa sare ya 1–1 ndani ya dakika 90 za kawaida, na hivyo kupelekwa moja kwa moja kwenye mikwaju ya penalti.
Matokeo ya mchezo:
⚽ 48’ Ghezala (goli la kujifunga – Algeria) akiwapa Sudan uongozi.
⚽ 73’ Bayazid akaisawazishia Algeria.
Katika mikwaju ya penalti, Sudan walionyesha utulivu na kutinga nusu fainali kwa ushindi wa 4–2.
Kwa matokeo hayo, Sudan sasa itakutana na Madagascar katika nusu fainali, huku mchezo mwingine wa nusu fainali utawakutanisha Morocco dhidi ya Senegal (Simba wa Teranga).