Kenya imeondolewa hatua ya robo fainali CHAN 2024

TIMU ya Taifa ya Kenya imefungashiwa virago kwenye CHAN 2024 katika hatua ya robo fainali mbele ya Madagascar kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Hawa ni majirani wetu na wenyeji wa CHAN 2024 ambapo mchezo wa leo Agosti  Uwanja wa taifa wa Moi mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa.

Kenya ilikuwa inapewa nafasi kubwa kusonga mbele imepoteza kwa penati ambapo baada ya dakika 90 ilikuwa Kenya 1-1 Madagagascar. Bao la Kenya lilifungwa na Alphonce Omija dakika ya 48 na Madagascar ni Fenohasina Gilles Razafiramaro dakika ya 69 kwa penati.

Dakika 30 ziliongezwa kwenye mchezo huo bado milango ilikuwa ngoma ngumu ndani ya dakika 120 hakuna mbabe, kwenye mapigo ya penati ilikuwa Kenya 3-4 Madagascar.

Mbinu za Kocha Mkuu,Benni Mccarthy zimegotea hatua ya robo fainali CHAN 2024 na Kenya ilikuwa moja ya timu imara kutoka ukanda wa CECAFA.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.