Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amempa kazi maalumu kiungo mkabaji wa Simba SC, Yusuph Kagoma kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Morocco.
Tayari hatua za makundi zimegota mwisho huku timu za Ukanda wa CECAFA zikiwa vinara katika makundi yao. Tanzania kutoka kundi B, Kenya kutoka kundi A na Uganda kutoka kundi C.
Tanzania ina kibarua cha kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali Agosti 22, Uwanja wa Mkapa na wapinzani wao katika CHAN 2024 ni Morocco.
Kamwe amesema: “Huu ni mchezo muhimu kwetu kushinda na wachezaji wana kazi kubwa kupambania ushindi. Nina amini yule mkabaji Yusuph Kagoma kazi yake iwe moja tu kuzuia njia zote za wapinzani kwa kushirikiana na wachezaji wengine, inawezekana.”
Mbali na Kagoma wachezaji wengine ambao wapo katika timu ya taifa ya Tanzania ni Clement Mzize, Dickson Job, Aishi Manula, Sopu mfungaji wa bao la kwanza kwenye CHAN 2024 kwa Tanzania.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.