INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba SC umekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Selemani Mwalimu.
Nyota huyo anatajwa kuwa muda wowote atajiunga na kikosi cha Simba SC, Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Kikosi cha Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kinaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 kikiwa nchini Misri.
Tayari uongozi wa Simba SC umetangaza siku ya tamasha lao la kuwatambulisha wachezaji na benchi la ufundi maarufu kwa jina la Simba Day ambayo itakuwa Septemba 10 2025.
Mshambuliaji huyo huenda ataungana na kundi ambalo linawahusisha mastaa wote, ambao wanaendelea na majukumu ya timu za Taifa kwenye mashindano ya Chan 2024 ambapo Tanzania ipo hatua ya robo fainali.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.