KATIKA CHAN 2024 ukuta wa timu ya Tanzania chini ya nahodha Dickson Job umeruhusu bao moja pekee ndani ya dakika 360.
Wakati ukuta ukizidi kuimarika, safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao matano kwenye mechi za ushindani.
Ilikuwa Tanzania 2-0 Burkina Faso, Agosti 2 2025, Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025 na Tanzania 2-1 Madagascar ilikuwa Agosti 16 2025.
Kete moja kupata pointi moja ilikuwa Central African 0-0 Tanzania, Agosti 16 2025. Mchezo huo ulikuwa ni wa nne kwenye hatua ya makundi.
Mwanzo wa maandalizi nchini Misri Job alibainisha kuwa wapo tayari na watapambana kufanya kweli katika mechi za ushindani.
Agosti 22 2025 ni Tanzania vs Morocco hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa. Kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali, Kocha Mkuu wa Tanzania, Hemed Suleman amesema kuwa watafanyia kazi eneo la umaliziaji ambalo limekuwa ni tatizo kwenye baadhi ya mechi.
“Tumekuwa tunatengeneza nafasi kwenye mechi zetu hilo lipo wazi ila katika umaliziaji hilo limekuwa ni jambo lingine. Nina amini kwamba kila kitu ni hatua wachezaji wanazidi kuwa imara na katika hatua ambayo tupo kwa sasa kinachohitajika ni matokeo,” amesema Suleman.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.