UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi siku mpya ambayo itakuwa ni maalumu kwa utambulisho mpya wa wachezaji wao na benchi la ufundi kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Kwa sasa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.
Msimu uliopita katika anga la kimataifa iligotea hatua ya fainali ikiwa nafasi ya pili mabingwa walikuwa ni RS Berkane iligotea nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Ni Septemba 10 2025 itakuwa ni siku rasmi ya Simba Day tamasha kubwa Afrika ambalo hutumika kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya, wale waliokuwa katika kikosi msimu uliopita na benchi la ufundi.
Miongoni mwa wachezaji wapya ndani ya Simba SC ni Jonathan Sowah ambaye ni mshambuliaji alikuwa ndani ya Singida Black Stars na alifunga mabao 13 kwenye ligi, Anthon Mligo beki wa kushoto alikuwa ndani ya Namungo FC, Naby Camara.
Wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya Simba SC miongoni mwao ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye ametambulishwa Yanga SC kwa kandarasi ya miaka miwili, Aishi Manula huyu atakuwa ndani ya Azam FC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.