LEONEL ATEBA KUACHWA SIMBA SC

INAELEZWA kuwa kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji wa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids huenda akaachwa katika kikosi hicho kuelekea msimu mpya.

Simba SC inatajwa kuwa kwenye mazungumzo ya kuachana na mshambuliaji huyo raia wa Cameroon, Lionel Ateba kutokana na kutoridhishwa na mwendo wake msimu uliopita.

Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo anajiandaa kuondoka kambini Cairo, Misri ambako kikosi hicho kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.

Ipo wazi kwamba msimu wa 2024/25 Ateba alifunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora kati ya mabao 69 yaliyofungwa na timu hiyo iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa “Taarifa rasmi ya klabu ya kutangaza wachezaji tutakaoachana nao na wapya hivi karibuni itatolewa,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.