UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa msimu mpya wa 2025/26 watafanya kazi kubwa kuleta ushindani kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge imeweka kambi nchini Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Miongoni mwa wachezaji wapya waliopo katika kikosi hicho ni Himid Mkami ambaye amerejea kwa mara nyingine kwenye viunga hivyo baada ya kuwa nchini Misri kwa muda wa miaka 7 akicheza soka la kulipwa nje ya nchi, Sadio Kanoute kiungo mgumu ambaye aliwahi kucheza Simba SC.
Thabit Zakaria, Mkuu wa Idara ya Habari Azam FC ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu mpya ni kuwa kwenye mwendo bora na kupata matokeo katika mechi za kitaifa na kimataifa.
“Mpango mkubwa ni kuwa imara na kuleta ushindani kwenye mechi ambazo tutacheza, tunatambua malengo makubwa ni kupata matokeo,wachezaji bora na kocha wa viwango ni mwanzo wa kuwa imara msimu ujao.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.