ALLAN OKELLO AKIWASHA UGANDA 2-O NIGER CHAN 2024

ALLAN Okello nyota wa timu ya taifa ya Uganda alifungua ukurasa wa magoli kwenye mchezo wa CHAN 2024. Ni Agosti 11 ilikuwa mbele ya Niger. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Uganda 2-0 Niger.

Goli la Okello ilikuwa dakika ya 25 ya mchezo. Goli la pili ni mali ya Joel Sserunjogi dakika ya 57. Wenyeji wa Michuano ya CHAN 2024, Kenya, Tanzania na Uganda wamekuwa kwenye mwendo mzuri katika hatua ya makundi.

Uganda wanaongoza kundi C wakiwa na pointi 6 baada ya mechi tatu. Algeria nafasi ya pili wana pointi 4. Afrika ya Kusini nafasi ya tatu wana pointi nne. Guinea nafasi ya nne pointi tatu huku Niger wakiwa nafasi ya tano hawajavuna pointi katika mechi mbili walizocheza.

Afrika Kusini walivuna pointi tatu mbele ya Guinea. Ilikuwa Afrika Kusini 2-1 Guinea. Magoli ya Afrika Kusini yalifungwa na Neo Gift Maema dakika ya 10 na Thabiso Simon Kutumela dakika ya 54. Goli la Guinea lilifungwa na Moussa Moise Camara dakika ya 37.

Kundi D leo Agosti 12 litakuwa kazini kwenye msako wa pointi tatu. Ni mechi za raundi ya pili ambapo mabingwa watetezi, Senegal watakuwa kibaruani dhidi ya Congo Brazzaville kusaka ushindi utakaowapeleka robo fainali kuanzia saa 11:00 jioni.

Kisha Nigeria waliopoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Senegal, watakuwa na kazi dhidi ya wabishi wa Sudan, wote wakisaka ushindi wa kwanza baada ya Sudan kutoka sare dhidi ya Congo hizi zitachezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.