SADIO Kanoute kiungo wa kazi ambaye aliwahi kucheza katika kikosi cha Simba SC muda wowote atatambulishwa na matajiri wa Dar Azam FC baada ya kukamilisha masuala ya vipimo ili awe hapo ndani ya msimu wa 2025/26.
Kaonoute tayari yupo kwenye ardhi ya Tanzania aliwasili Agosti 10 2025 kwa ajili ya kukamilisha masuala ya usajili ndani ya Bongo kwa mara nyngine tena.
Mara baada ya kuwasili alisema“Nina furaha kuwa hapa, kuwa Azam, najisikia nipo nyumbani. Nitafanya kadri niwezavyo kuwafanya mashabiki wa Azam FC wawe na furaha.”
Maneno ya kiungo wa soka Sadio Kanoute, alipozungumza baada ya kuwasili Dar kwa ajili ya kujiunga na Azam FC.
Kanoute ni moja ya viungo imara kwenye eneo la ukabaji, mara chache kumuona akionyesha tabasamu akiwa uwanjani zaidi ya ile mikato ya kimyakimya. Akikamilisha vipimo na kusaini mkataba ataibukia Karatu kujiunga na wenzake wa Azam FC ambao wameweka kambi huko.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.