TANZANIA 2-1 MADAGASCAR, ROBO FAINALI CHAN 2024 REKODI MPYA

TIMU ya taifa ya Tanzania imeandika rekodi mpya kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika CHAN 2024.

Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar umefungua njia kwa Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Suleiman.

Mabao ya Tanzania yote mawili yamefungwa na Clement Mzize dakika ya 13 na 20 huki bao la Madagascar likifungwa na Nantenaina Razafimahatana dakika ya 34.

Tanzania inaongoza kundi B ikiwa na pointi tisa mechi zote tatu imeshinda huku ikifunga jumla ya mabao matano na kuruhusu bao moja pekee.

Shukrani kwa Dickson Job nahodha wa Tanzania kuiongoza safu ya ulinzi kwa umakini akishirikiana na wachezaji wote ikiwa ni Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Ibrahim Bacca katika eneo la ulinzi.

Kwenye mchezo wa mapema wa kundi B, Afrika ya Kati 0-1 Mauritania ambao walifungwa na Tanzania mchezo uliopita.

Bao la Mauritania lilifungwa na Ahmed Ahmed dakika ya 9 ilikuwa Uwanja wa Mkapa. Mechi ya Tanzania ilianza saa 2:00 usiku, Agosti 9 2025.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.