HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA SC ANGA LA KIMATAIFA

KWENYE anga la kimataifa Simba SC ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali itacheza dhidi ya Gaborone United ya Botswana.

Simba SC msimu wa 2024/25 ilikuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Msimu wa 2025/26 itakuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Baada ya droo michuano ya CAF ngazi ya klabu CAF CL na CAF CC kufanyika leo Agosti 9 2025 tayari wameshawatambua wapinzani wao.

Droo hiyo imechezwa katika studio za Azam TV, Dar ni droo ya hatua za awali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba SC itaanzia ugenini na kukamilisha kete ya pili ikiwa nyumbani. Kato ya Septemba 19-21 ugenini na kati ya Septemba 26-28 ikiwa nyumbani.

Kikosi cha Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwa sasa kipo Misri kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.