KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemedi Selemani, amesema kuwa ana imani kubwa na kikosi kuelekea mchezo unaofuata wa Agosti 6, 2025 dhidi ya Mauritania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Kocha huyo amesisitiza kuwa lengo kuu ni kupata ushindi bila kujali idadi ya mabao kwenye mchezo wa leo unaotarjiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Suleiman amesema kuwa ushindi ndio jambo la msingi zaidi katika mashindano ndani ya uwanja jambo ambalo wanalitarajiwa baada ya dakika 90 za mchezo.
“Naamini sana katika kupata ushindi haijalishi tutafunga magoli mangapi cha msingi ni kupata ushindi. Wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wetu muhimu na tunawaheshimu wapinzani wetu.”
Tanzania kwenye mchezo wa kwanza ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso, mabao yalifungwa na Sopu na Mohamed Hussen Zimbwe Jr.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.