MOHAMED HUSSEN ZIMBWE JR NI NJANO NA KIJANI

USIKU wa kuamkia Agosti 6 2025, Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyekuwa nahodha wa Simba SC 2024/25 ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Yanga SC.

Zimbwe Jr beki wa kazi ndani ya Simba SC msimu wa 2024/25 upande wa kushoto alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Fadlu Davids.

Anatambulishwa Yanga SC akiwa mchezaji huru kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umegota mwisho ndani ya Simba SC na hakuongeza mkataba mpya kutokana na maslahi ya pande zote mbili kwa Simba SC na mchezaji mwenye Zimbwe Jr.

Msimu wa 2024/25 rekodi zinaonyesha kuwa Zimbwe Jr katika kikosi cha Simba SC alicheza jumla ya mechi 27 kati ya 30 za Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC ambayo ni namba nne kwa ubora.

Alihusika kwenye mabao matano, alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga na alitoa jumla ya pasi nne za mabao.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.