MSHAMBULIAJI WA MABAO YANGA SC AUZWA UARABUNI

INAELEZWA kuwa Yanga SC wamefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wa mabao ndani ya kikosi hicho ambaye ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi msimu wa 2024/25.

Ni Clement Mzize ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Mzize anashikilia rekodi ya kucheza mechi zote 30 za ligi msimu uliopita.

Mshambuliaji huyo alifunga jumla ya mabao 14 akiwa anaongoza chati ya wafungaji wazawa. Mshambuliaji namba moja ni Jean Ahoua wa Simba SC ambaye alifunga mabao 16 kibindoni.

Taarifa zinaeleza kuwa mezani Yanga SC itavuna Dola 900,000 (Sawa na Sh 2.2Bil) kumuuza Klabu ya klabu ya Al-Sadd SC ya nchini Qatar.

Inaelezwa kuwa Yanga wamekubali kumuuza Mzize, lakini menejimenti ya mchezaji huyo wanataka mshahara wa Dola 50,000 (Sawa na Sh 124.7Mil) kwa mwezi.

Mzize kwenye ligi baada ya kucheza mechi 30 alikomba dakika 1,877 msimu wa 2024/25. Bao la 14 alifunga kwenye Kariakoo Dabi Juni 25 2025 alipowatungua Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.