BAADA ya kutambulishwa katika Klabu ya USM Algers ya nchini Algeria beki Fondoh Che Malone ameanza mazoezi katika kikosi hicho.
Beki huyo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye mechi za ligi ilikuwa Uwanja wa KMC, Mwenge Dar.
Katika mchezo huo Che Malone alifungua ukurasa wa mabao kwa kutumia pasi ya kiugo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye ni namba moja kwa kufunga mabao mengi akiwa nayo 16 kibindoni.
Che Malone ambaye alifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo dhidi ya Tabora United dakika ya 13 kwa pigo la kichwa wiki hii alitambulishwa USM Algers ambako Simba SC ilimuuza baada ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kumuhitaji baada ya kuonyesha kiwango kikubwa.
Che Malone anachukua nafasi ya Kelvin Mondeko ambaye mkataba wake ulivunjwa baada ya makubaliano ya pande mbili.
Julai 30 2025, Che Malone alipewa Thank You na Simba SC ambayo imeweka kambi nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.