YANGA YAMTAMBULISHA CÉLESTIN ECUA KUTOKA IVORY COAST

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliji Célestin Ecua, raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 23, kama mchezaji mpya wa kikosi chao kwa msimu ujao, akitokea klabu ya Zoman FC ya nchini kwao.

Ecua alikuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita akiwa na Zoman FC, ambapo alifunga magoli 15 na kutoa ‘assists’ 12 katika michuano yote aliyoshiriki. Uwezo huo ulimuwezesha kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) nchini Ivory Coast.

Kwa ujio wake, safu ya ushambuliaji ya Yanga SC inaendelea kuimarika zaidi, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki michuano ya ndani na kimataifa kwa mafanikio makubwa.