ISRAEL Mwenda beki wakupanda na kushuka bado atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz nakufanya kuwa na wapya wanne ndani ya Julai 29 waliotangazwa Yanga SC.
Mwenda alitambulishwa Yanga SC kwenye dirisha dogo akitokea Singida Black Stars kwa mkopo kutokana na kuwa kwenye kiwango bora mabosi wa Yanga SC wamemuongezea kandarasi kuendelea kuwa Jangwani.
Kwa msimu wa 2025/26 ni uhakika atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi baada ya kutwaa taji hilo msimu wa 2024/25.
Mbali na Mwenda kutambulishwa kuwa atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu ujao kuna wengine wapya watatu waliotambulishwa Yanga SC, Julai 29 2025 ikiwa ni Tshephang Mokaila huyu ni fitnes coach.
Mkurugenzi wa Ufundi, Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025 na Manu Rodriguez huyu alitambuliwa kuwa ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.